Wanachama wa Simba wapokea katiba mpya kinyonge

Wanachama wa Simba wapokea katiba mpya kinyonge



Baadhi ya wanachama wa Simba wameipokea katiba mpya ambayo imetoka kusajiliwa hivi karibuni na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa katika makao makuu ya klabu hiyo.

Licha ya kuipokea katiba hiyo, wanachama hao wamepingana na baadhi ya vipengele ambavyo wameeleza kuwa havikuwa katika makubalino ya pande mbili baina ya viongozi na upande wao.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwanamachama mmoja anayejulikana kwa jina la Mussa Said kutoka tawi la Simba Tishio, amesema kuwa kipengele cha kumtaka mgombea Urais kuwa na kiwango cha elimu ya shahada haikujadiliwa pamoja.

Aidha ameeleza pia kipengele kingine ni kuhusiana na kuhusiana na wajumbe ambao wanapaswa kuwa na elimu ya kiwango cha elimu ya kidato cha nne, akisema kuwa si jambo sahihi.

Wakati Said akilalamikia na kuhoji juu ya katiba hiyo iliyosajiliwa mwaka huu 2018, malalamishi yake yanakuwa kama ynakosa nguvu kutokana na Msajili Mkuu kutoka Serikalini, Mkwawa, kuipitisha katiba hiyo kuwa ndiyo itatumika kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Klabu ya Simba kupitia viongozi wake watakutana Agosti 31 kwa ajili ya kuandaa Kamati maalum ya Uchaguzi kuanza mchakato rasmi wa kuwapata viongozi watakaoweza kuiongoza klabu kwa miaka minne ijayo.

Post a Comment

0 Comments