Wapanda milima na watalii 16 wafariki dunia na 300 kujeruhiwa kwenye tetemeko la ardhi

Wapanda milima na watalii 16 wafariki dunia na 300 kujeruhiwa kwenye tetemeko la ardhi



JUMLA ya wapanda milima na watalii 16 wamekufa na wengine 300 wamejeruhiwa baada ya kunaswa kwenye tetemeko la ardhi visiwa vya nchini Indonesia.

Pia, wapo wapanda milima wasiopungua 500 wamekwama, baada ya kunasa kwenye tetemeko la ardhi kwenye milimani ya visiwa vya Indonesia, shughuli za kuwashusha zikiendelea.

Ni tetemeko lililotokea katika Mlima Rinjani, baadhi walinusuriwa na helikopta kutoka milimani na juhudi nyingine zinaendelea kuwanasua waliokwama, akiwemo mtalii. 

Msemaji wa serikali anayehusika na majanga, Sutopo Purwo Nugroho, anasema watu 543 waliokuwa wakipanda mlima, walishashuka Jumatatu iliyopita.

Pia, upande wa makazi, kuna mamia ya watu hawana makazi kutokana na tetemeko hilo.

Indonesia ni eneo ambalo liko rafiki kuhusiana na tetemeko la ardhi, ambalo huwa linatokea kila mara na jamii hii sasa inachukua hatua ya kurejesha majengo ya umma na miuundombinu ya mahitaji muhimu kama vile umeme.BBC

Post a Comment

0 Comments