Afande Sele amchambua Alikiba na Diamond

Afande Sele amchambua Alikiba na Diamond


Msanii mkongwe wa muziki, Afande Sele amefunguka kwa kudai kuwa katika utafiti wake mdogo alioufanya amegundua Alikiba ana mashabiki wengi mjini huku Diamond akidai anapendwa sana vijijini.

Wawili hao wamekuwa kwenye ushindani wiki hii baada ya kila mmoja kuachia wimbo mpya huku wimbo wa Alikiba, Seduce Me ukionekana kufanya vizuri mtandaoni.

Wasanii na viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakitoa pongezi kwa kila msanii.

Kwa upande wa rapa Afande Sele ametoa uchambuzi mdogo kuhusu wasanii hao baada ya kuonekana kushindanishwa sana mitandaoni.

Kupitia instagram, Afande aliandika

“Juzi Kati Nilipokua Kiteto Ndipo Nikasikia Habari Ya Kwamba Kiba Na Chibu Wote Wametoa Ngoma Mpya…Lkn Baada Ya Hapo Kuanzia Pale Kiteto Na Maeneo Yote Ya Vijiji Na Miji Niliyokua Napita Wkt Wa Kurudi Moro Nikawa Nausikia Wimbo Wa Chibu Tu Aliowashirikisha Wadogo Zake Ingawa Mimi Kama Mdau Wa Mziki Nilikua Ninashauku Ya Kuusikia Wimbo Wa Kiba Pia….Nilishindwa Kuingia Mitandaoni Kuutafuta Kwakua Nilikua Naendesha Gari Muda Wote Wa Safari Hivyo Nilivumilia Hadi Nilipofika Nyumbani Ndipo Nikazama Mitandaoni Ambapo Huko Nilishangaa Kukuta Hali Ni Tofauti Kabisa Na Ilivyo Mitaani Hasa Kule Vijijini….Wkt Huko Mitaani Habari Kuu Ni Wimbo Wa Chibu…Huku Mitandaoni Habari Kuu Ni Wimbo Wa Kiba….Hapo Nikajifunza Kitu Kwamba Inawezekana Kuwa Kiba Anakubalika Zaidi Na Watu’fulani’Wa Mjini Halafu Chibu Anakubalika Sana Na Watu Wa’kawaida’Ktk Maeneo Yote Hasa Vijijini….Kwa Kuzingatia Hilo Nikagundua Kuwa Kibiashara Na Kick Za Kijamii Chibu Yupo Vizuri Zaidi Tofaut Na Kiba Ambae Kiheshima Na Utanashati Yupo Juu Wkt Wote….Jambo Muhimu Nililoliona Kwa Wote Ni Kwamba Kila Mmoja Anakitu Cha Kujifunza Kwa Mwenzake….Chibu Anaweza Kujifunza Utulivu…Usikivu Na Umakini Wa Hali Ya Juu Alionao Kiba Ktk Kupangilia Kazi Zake Kutoka Hatua Za Awali Mpaka Anapozitoa Hewani…Yeye Kiba Anayo Nafasi Ya Kujifunza Kuwa Timu Nzuri Ni Ile Inayofanya Usajili Mzuri Na Yenye Kufanya Mikakati Ya Ushindi…Nje Ya Mziki Ally Kiba Ni Mwanasoka Bila Shaka Anafahamu Falsafa Ya Mpira Pasi Mziki Pia Upo Hivyo…Zaidi Ya Vyote Nawapongeza Wote Kama Wadogo Zangu Na Wasanii Hodari Wa Nyakati Hizi Ingawa Nawapa Angalizo Kuwa Waendelee Kukomaa Kwani Wao Sio Wasanii Wazuri Kuliko Wote Ingawa Wanapewa Nafasi Kuliko Wote…Huo Ni Mtazamo Wangu Mimi Tu Wala Sio Sheria…Zaid Ya Hapo”Wacha Nilewe…Nilewe Tuu”….

Post a Comment

0 Comments