Taarifa za wahalifu kwangu ni mtaji – Kamanda Mambosasa

Taarifa za wahalifu kwangu ni mtaji – Kamanda Mambosasa


Baada ya IGP Simon Sirro Kumteua, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lazaro Mambosasa kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.Leo kwa mara ya kwanza amezungumza na kusema kuwa taarifa za wahalifu na uhalifu ni mtaji utakao mfanya ajue mahali gani pa kukanyaga.


Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa ambapo ameomba ushirikiano na wananchi wa jiji la Dar es salaam.

“Nimeteuliwa nije kwenu na amenituma kabla ya kufanya chochote nikutane nanyi niwaombe ushirikiano katika kupashana habari lakini katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mwisho wa siki mimi na nyie na nikisema nyie namaanisha wakazi wote wa Dar es salaam nataka tupafanye Dar es salaam pawe mahali salama pa kuishi,” amesema Kamanda Mambosasa.

“Ninajua hayo hayawezi kufanyika bila ushirikiano wa wananchi ndio maana nimetokea kupitia kwenu kuomba ushirikiano wa dhati kwa wananchi wote wa Dar es salaam mimi ninachoomba kutoka kwenu ni taarifa tu na kwangu taarifa za wahalifu na uhalifu ni mtaji utakao nipa platform ni mahali gani pa kukanyaga ili niweze kupaa na Kanda maalum ya Dar es salaam.”

Post a Comment

0 Comments