Floyd Mayweather amethibitisha kuwa bondia asiyepigika baada ya kumshinda kwa TKO dhidi ya Conor McGregor katika round 10 ambapo baada ya mchezo huo bondia huyo alisisitiza kuwa hatopigana tena.
Kwa ushindi huo Mayweather anakuwa amecheza mapambano 50 na hajapoteza hata pambano moja na ameweka wazi kuwa hatopigana tena.
Pambano hilo lilishuhudiwa na watu wapatao 20,000 katika ukumbi wa T-Mobile Arena, Las Vegas miongoni mwao wakiwa mastaa wa filamu, muziki na watu maarufu ambao walisafiri kwenda kuushuhudia ambapo miongoni mwao ni Bruce Willis, Leonardo DiCaprio, Jennifer Lopez, Vanessa Hudgens, Demi Lovato na LeBron James.
Mwigizaji na mwanamuziki Jennifer Lopez na mchezaji wa zamani wa MLB Alex Rodriguez
Leonardo DiCaprio
Bruce Willis akifuatilia pambano
Mastaa LeBron James na Mike Tyson wakifuatilia kwa makini pambano
Mwigizaji staa kutoka Hollywood Gerard Butler naye hakukaa nyumbani
Mwigazji Chris Hemsworth alikuwepo kwenye pambano Mayweather vs McGregor
LeBron James akishuhudia pambano Mayweather vs McGregor. Nyuma ya staa huyo wa Cleveland Cavaliers ni Mike Tyson
P Diddy
Jamie Foxx, akiwa T-Mobile Arena, Las Vegas
Mwigizaji Charlize Theron akifuatilia kwa makini Floyd Mayweather Jr. vs Conor McGregor
Mmiliki wa NFL Robert Kraft alisafiri kwa ndege binafsi akiwa na J-Lo na A-Rod
Cedric The Entertainer (kushoto) na Akon hawakubaki nyumbani
0 Comments