Wachezaji wa timu ya Liverpool wakicheza muziki baada ya kuwapa kipigo cha nguvu timu ya Arsenal cha bao 4-0 mchezo huo uliopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Anfield.
Liverpool imeifanya kitu kibaya Arsenal baada ya kuitandika mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Premier League.
Arsene Wenger (kulia) akiwa hoi baada ya kupokea kichapo cha bao tatu mubashara.
Katika mchezo huo uliopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Anfield, Arsenal ilionekana kuzidiwa kuanzia mwanzoni mwa mchezo na kujikuta ikipoteza kwa idadi hiyo ya mabao ambayo imekuwa ni rekodi mbaya kwa mashabiki wa Arsenal ndani ya msimu huu wa 2017/18.
Wafungaji katika mchezo huo ni Roberto Firmino katika dakika ya 17, Sadio Mane dakika ya 40, Mohamed Salah (73) na Daniel Sturridge aliyeingia akitokea benchi kipindi cha pili akatupia katika dakika ya 77.
Katika mchezo huo Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alimchezesha Alexis Sanchez kwa mara ya kwanza msimu huu tangu arejee klabuni hapo akitokea katika mapumziko.
Sanchez hakuonyesha kiwango kizuri, alitolewa dakika ya 62 na nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud ambapo Sanchez alionekana akiwapungua mashabiki mkono kama mtu anayewaaga.
0 Comments