Dawasa yajipanga kuboresha huduma

Dawasa yajipanga kuboresha huduma



Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Romanus Mwang'ingo 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) imesema imeandaa miradi ya kuboresha upatikanaji wa maji nchini na uondoaji wa maji taka.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Romanus Mwang'ingo amesema miradi hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wa kawaida na wenye viwanda na biashara wanapata huduma bora.

Amesema pia, wana mkakati wa kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kwa kufunga mita maalumu maeneo ya upokeaji maji na katika matoleo ili kujua kiasi kamili kinachoingia katika eneo husika na kilichogawanywa kwa wananchi.

Miradi ya ujenzi wa mitambo mikubwa ya kisasa ya kusafisha maji taka itatekelezwa pamoja na kulaza mabomba maeneo ya Jangwani, Mbezi Beach na Kurasini.

Mwang'ingo amesema miradi mikubwa ya maji katika miji ya Mkoa wa Pwani inayotekelezwa na Dawasa ni ya Kibiti, Ikwiriri, Chalinze, Mkuranga, Kisarawe na Kilindoni (Mafia).

Amesema kati ya hiyo, ipo ambayo imeshakamilika na tayari inahudumia wananchi.


Post a Comment

0 Comments