Timu ya Arsenal ya nchini Uingereza hapo jana ilikubali kipigo kizito cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool ambayo ilikuwa nyumbani Anfield.
Kufuatia matokeo hayo Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani na timu hiyo baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha.
Wenga amesema kuwa matokeo hayo yanadhihirisha wazi kuwa bado hawapo imara
“Kwa matekeo haya yanatosha kudhihirisha kuwa bado tunakazi ya kufanya ila wapo baadhi ya watu wanahisi kwamba mimi ndiye kikwazo, basi naomba radhi kwamba mimi ndiye tatizo,” Wenger aliambia Sky Sports.
Arsene Wenger ameongeza “Tunachohitaji mashabiki wetu waendelee kuwa nasi hata baada ya uchezaji mbaya na kushindwa”.
Magoli ya Liverpool yakifungwa na Roberto Firmino dakika ya (17) na Sadio Mane (40) wakati mengine yakifungwa katika kipindi chapili na Mohamed Salah kunako dakika ya (57) pamo na Daniel Sturridge (77)
Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano msimu uliyopita na hivyo kushindwa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.
0 Comments