RC Makonda awaonya Alikiba na Diamond Platnumz

RC Makonda awaonya Alikiba na Diamond Platnumz


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amefurahishwa na ushindani wa kimuziki baina ya Diamond Platnumz na Alikiba kwa kusema unachangamsha muziki wetu huku akiwaonya kuwa kazi zao lazima wazingatie sheria na maadili yetu.

Mhe Paul Makonda

Mhe Makonda amesema anapenda sana anavyowaona vijana hao wakishindana na ushindani wao unafanya muziki ukue kwa kufanya kazi nzuri.

“Tofauti zenu mimi nazipenda, kwani zinaleta ushindani mzuri kwenye mziki“,ameandika Mhe Paul Makonda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwaonya kuwa ni lazima wazingatie sheria na utamaduni wetu kwenye kazi zao kwa kusema “Ila naomba mzingatie sheria na Utamaduni wetu..“.

Alikiba kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Seduce Me huku Diamond Platnumz akifanya vizuri na nyimbo zake kama Fire, Eneka, I miss u na ule mpya wa ‘Zilipendwa’ ambao umeimbwa na wasanii wote wa WCB

Post a Comment

0 Comments