Mhe Tundu Lissu atangaza mgomo

Mhe Tundu Lissu atangaza mgomo


Mwanasheria mkuu wa CHADEMA na Rais wa chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Mhe Tundu Lissu, amewataka mawakili wote nchini kugoma kwenda mahakamani siku ya jumanne na jumatano, kuonesha kupinga vitendo walivyofanyiwa mawakili wenzao wa IMMMA, ambao ofisi yao imechomwa moto.

Mhe Tundu Lissu katikati

Tundu Lissu amesema kitendo hicho kinaingilia uhuru wa wanasheria na taaluma ya sheria pia kinahatarisha uhuru wa mahakama na utawala wa sheria kwa ujumla huku akiwataka mawakili wote nchini walio chini ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kutokwenda mahakamani kufanya kazi zao.

“Baraza la uongozi linawataka wanachama wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria katika mahakama pamoja na mabaraza ya aina zote kati ya siku za jumanne na jumatano ya tar 29 na 30 Agosti 2017, kwa lengo la kuwaunga mkono mawakili wa IMMMA, na kuonyesha kutokukubaliana kwetu na vitendo vya kihalifu vya kuwashambulia mawakili hao kwa mabomu”, amesema Mhe Tundu Lissu leo kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Post a Comment

0 Comments