Mimi na Weusi hatuna beef – Nisher

Mimi na Weusi hatuna beef – Nisher


Director wa music video Bongo, Nisher amesema uhusiano wake na kundi la Weusi upo vizuri.


“Mimi na G Nako hatuna beef, mimi na kampuni nzima ya Weusi hatuna beef. Nimetoa Choro Joh Makini amenipa pongezi, hamna chochote kibaya kati yetu,” Nisher amesema hayo wakati akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii.

“Joh Makini ametoa kazi yake juzi Kata Leta na Davido, very classic video. Nampenda kila mtu, sio mtu wa beef, siwezi beef, naweza zaidi kuwa productive,” ameongeza.

Video za Weusi alizofanya Nisher ni kama Nje ya Box, XO na Sijuti za Joh Makini, Mama Yeyoo ya G Nako n.k.

Post a Comment

0 Comments