Roma hakurupuki kuachia ngoma – Dayna Nyange

Roma hakurupuki kuachia ngoma – Dayna Nyange


Kutokana na ukaribu wake wa kifamilia na Roma, msanii wa Bongo Flava Dayna Nyange amesema rapper huyo huwa hakurupuki kuachia ngoma kutokana na kile ambacho anaandika.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’, amesema kutokana na hilo huwa hana wasiwasi anaposikia Roma anataka kutoa wimbo.

“Ukimuangali Roma ni mwanamuziki yupo tofauti na watu wengi, yaani hata huwezi kuanza na kumlinganisha na mtu mwengine kwa sababu ya aina ya muziki ambao ameuchagua, I know him, yupo vizuri kichwani, ana uwezo, anajielewa na yupo makini,” Dayna ameiambia Bongo5.

“Watu wanajua Roma ni mtu ambaye haogopi chochote lakini kwenye kazi zake ni mtu ambaye anakuwa na uogo, hakurupuki kuachia kazi, mpaka aamua asema hii inatoka,” ameongeza.

Roma kwa sasa anatamba na ngoma yake ‘Zimbambwe’, ngoma hii ilitoka August 10 hadi sasa ina views 1,283,106 katika mtandao wa Youtube.

Post a Comment

0 Comments