Klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imekataa ofa ya paundi milioni 25 ya Chelsea kumsajili mchezaji wao, Ross Barkley.
Barkley kiungo huyo wa timu ya taifa ya Uingereza atalazimika kuuzwa na Everto kabla ya dirisha la usajili kufungwa siku ya Alhamisi ili kuepusha kuondoka bure msimu ujao ambapo mkataba wake unafikia kikomo.
Everton wanahitaji dau la paundi milioni 50 ilikumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa maiaka 23 huku klabu ya Tottenham ikiingia katika mbio za kunasa saini yake.
0 Comments