The Gunners wagoma kumtoa Sanchez

The Gunners wagoma kumtoa Sanchez


Kiasi cha paundi milioni 50 cha Manchester City kumsajili mshambuliaji, Alexis Sanchez kimekataliwa na klabu ya Arsenal.


Sanchez mwenye umri wa maiaka 28 ameifungia Arsenal mabao 24 katika msimu uliyopita anahitaji kukichezea kikosi cha Meneja, Pep Guardiola lakini inaonekana kuwepo na kikwazo kutoka ndani ya klabu yake.

Arsenal wamezungumza na Sanchez ili asalie katika kikosi hicho bila mafanikio na hivyo wanahitaji Raheem Sterling kuwa sehemu ya mkataba wa mchezaji wao Kujiunga na City kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya Alhamisi.

Sterling raia wa Uingereza mwenye umri wa maiaka 22, amecheza katika michezo mitatu ya msimu huu ambayo City imeingia uwanjani.

Inaaminika Sterling anavutiwa kurudi katika mji aliyo zaliwa wa London hivyo huwenda dili la Sanchez kuamia City likafanikiwa.

Sanchez alijiunga na Arsenal akitokea Barcelona alipokuwa chini ya Guardiola mwaka 2014 kabla ya kuuzwa kwa paundi milioni 35.

Post a Comment

0 Comments