KRC Genk yalazimishwa sare 1-1

KRC Genk yalazimishwa sare 1-1


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo alikuwepo uwanjani, Luminus Arena mjini Genk kwa dakika zote, timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy alianza kuifungia Genk dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji Mbelgiji, Zinho Gano kuisawazishia KV Oostende dakika ya 74.

Huo unakuwa mchezo wa 64 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari mwaka jana alipojiunga na Genk, akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka jana alipokuwa na Mazembe, 37 alianza na mechi 24 alitokea benchi.

Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo wa zamani wa African Lyon, zamani Mbagala Market na Simba zote za Dar es Salaam, amefunga jumla ya mabao 21 kwenye mashindano yote.

Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Vukovic, Mata, Aidoo, Colley, Nastic, Benson/Buffalo dk86, Malinovskyi/Ingvartsen dk75, Pozuelo, Berge, Writers na Samatta.

KV Oostende: Vanhamel, Lombaerts, Siani, Berrier/Vandendriessche dk45, Musona, Jali, Bjelica, Rezaeian/Capon dk62, Tomasevic, Milic na Gano/Akpala dk84.

Post a Comment

0 Comments