Maradona aanza kibarua kipya kwa mbwembwe

Maradona aanza kibarua kipya kwa mbwembwe

Gwiji la soka nchini Argentina, Diego Maradona ametua kwa mbwembwe nchini Belarus kuanza kazi yake mpya kama Mwenyekiti wa klabu ya Dinamo Brest FC.


Maradona ametua nchini Belarus huku akitumia gari ya kifahari aina ya Mercedes Benz kabla ya kuhamishiwa katika usafiri mwingine ambapo alitambulishwa rasmi na mashabiki.

Diego Maradona mwenye umri wa miaka 57 aliiwezesha Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka 1986 lakini pia akiifundisha timu yake ya taifa mwakka 2008 – 2010.

Kupitia tovuti ya klabu ya Dinamo Brest imeeleza kuwa gwiji huyo atakuwa mwenyekiti na wala siyo kocha kama wengi walivyotarajia lakini pia kuangazia maendeleo ya soka la vijana.

Post a Comment

0 Comments