Sadio Mane akabidhiwa namba ya Coutinho, Salah aonyesha uwezo kwenye kikapu

Sadio Mane akabidhiwa namba ya Coutinho, Salah aonyesha uwezo kwenye kikapu

Nyota wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane wamerejea hii leo siku ya Ijumaa huko Melwood tayari kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza.

Mane raia wa Senegal amekabidhiwa jezi na 10 ambayo alikuwa akiiva Mbrazil, Philippe Coutinho aliyetimkia FC Barcelona na kuachana namba 19 aliyokuwa akiitumia toka alipotoka Southampton mwaka 2016.


Jezi namba 10 ndani ya Liverpool imewahi kuvaliwa na wachezaji kama, John Barnes, Joe Cole, Luis Garcia, Michael Owen na Andriy Voronin.


Mane na Salah walikuwa kwenye michuano ya kombe la dunia ambapo waliwakilisha mataifa yao.

Post a Comment

0 Comments