Zari awapiga STOP Wema na Aunty Ezekiel kwenda Afrika Kusini kwenye Birthday ya Tiffah

Zari awapiga STOP Wema na Aunty Ezekiel kwenda Afrika Kusini kwenye Birthday ya Tiffah


Baada ya mwanamuziki Diamond Platnumz kualika watu takribani 50 kuuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mtoto wake Tiffah, mzazi mwenzake, Zari Hassan amepiga marufuku ugeni huo.


Awali Diamond aliahidi kuwalipia tiketi watu 30 kwaajili ya kuhudhuria sherehe hizo lakini baadaye aliongeza kuwa atawalipia watoto 10 pamoja na wazazi wao ili nao wahudhurie sherehe hizo.


Katika kunogesha sherehe hizo, jana wakati wa sherehe ya kufikisha siku 40 ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema, mwanamuziki huyo alialika wanakamati zaidi ya 10 kuhudhuria sherehe hiyo.


Hata hivyo, Zari katika mtandao wa Instagram aliandika kuwa hautaki ugeni huo akihofia kuchafuliwa nyumba yake: “Sitaki kunichafulia nyumba kaeni hukohuko.”


Miongoni mwa wanakamati walioalikwa ni Wema Sepetu ambaye amewahi kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz na mwigizaji Aunty Ezekiel.


Tiffah ambaye jina lake halisi Latiffah alizaliwa Agosti 6, 2015. Hata hivyo sherehe za kuzaliwa binti huyo zitafanyika siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 17- 19 mwaka huu.

ad

Post a Comment

0 Comments