DALILI ZA MAHUSIANO YENU KUVUNJIKA

DALILI ZA MAHUSIANO YENU KUVUNJIKA


Najua wengi wetu tayari tulishawai kuwa kwenye mahusiano na wengine tuko kwenye mahusiano kwa sasa basi kwa leo hii inakuhusu ambapo tunaangalia Hatua zinazoonyesha penzi limepoteza muelekeo na kwenda kuachana.


MAWASILIANO KUWA DUNI
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara nyingi kama tano kwa siku (kwa wale walio mbali.), na ukiona yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho wa siku mawasiliano kukata kabisa. Na kila mmoja akiulizwa swali kwanini anasema nilibanwa na kazi basi hii ni hatua mbaya sana na hii huwa na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine.


HASIRA ZA MARA KWA MARA.
Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha ni kama unamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti.


KUZUNGUMZA MANENO YASIYOFAA MUWAPO PAMOJA
Hii ni hatua ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Mpenzi wako hutamuona mchungu kupita kiasi. ukishaona mke wako mara nyingi yeye na wenzake, hana muda na wewe basi ujue kuna jambo linaendelea ambolo mwisho wake ni kutengana.


KUDAI KUTENGANA KILA MARA
Hii ni hatua ya mwisho kabisa na Hapa mpenzi wako utaona ni balaa tupu. Yaani hafai hata kidogo. Kama una imani ndogo utatamani uondoke uende mbali ambako hutamwona tena. Hapa hakuna jinsi na usipofanya kama atakavyo mpenzi wako unaweza kuishia hata gerezani au kuchukua uamuzi wa kumpiga.


ZINGATIA
Kama bado unampenda unapaswa kwenda kuomba msamaha kwa yule uliyemwacha. Kukataliwa kwa mara ya kwanza ni jambo la kawaida, kwani ile picha itaendelea kumrudia. Jifanye kama usikii, fanya hivi zaidi ya mara tano hadi kumi. Mke wako au mme wako ataanza kukuonea huruma na hatimae kuwa naye pamoja

Post a Comment

0 Comments