Jana July 31, 2018 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe alitoa majibu baada ya kutakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuripoti kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi kwa kufanya mkutano katika Jimbo lisilo lake nakusema Waziri hana mamalaka hayo kisheria.
Muda mfupi baada ya Zitto kujibu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema nae akatoa neno kuhusiana na kauli ya Zitto.
Namnukuu Lema “Zitto, Waziri Kange anaweza kuwa hana Mamlaka kisheria lakini nikukumbushe kuwa siku hizi mambo yanaendeshwa kwa mizuka na matamko, kwa bahati mbaya Polisi wameshindwa kushinda jaribu hili. Kwa hali ilivyo sasa Jokate anaweza kumweka Pinda mahabusu na wakapiga makofi”
0 Comments