Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Afrika kusini inaendelea kuhakikisha kuwa na mpango wake wa kurekebisha katiba ili waweze kuchukua ardhi bila fidia,
Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa alisema kuwa chama cha ANC, kitahakikisha wanamalizia marekebisho ya katiba ili kuwezesha zoezi hilo kuanza.
Ramaphosa amesema kuwa mabadiliko hayo ni muhimu sana katika maendeleo ya uchumi nchini humo siku za hivi karibuni kumekua na malalamiko makubwa juu ya mabadiliko hafifu ya masuala ya ardhi Afrika kusini.
Watu weupe ambao ni idadi ndogo ya raia wa Afrika kusini wanaaminika kuwa ndio wanashikilia maeneo makubwa ya ardhi na yenye rutuba.Wakoasoaji wa suala hili wanasema kuwa inaweza kuwa kama nchi jirani ya Zimbabwe na ikawa ni upokonyaji wa ardhi.
Karibu asilimia 10 ya ardhi inayomilikiwa na watu weupe imegaiwa kwa watu weusi tangu kuisha kwa sera ya ubaguzi wa rangi (apartheid), suala ambalo ni theluthi tu ya lengo la ANC
0 Comments