Kampuni ya SBC yarudisha faida waliyoipata kwa jamii

Kampuni ya SBC yarudisha faida waliyoipata kwa jamii



Na James Timber, Mwanza
Kampuni ya SBC Tanzania Limited, wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa vinywaji baridi aina ya Pepsi, Mirinda, 7 up, Mountain Dew na Everveness, mkoani Mwanza wamerudisha faida wanayoipata kwa jamii kutokana na biashara yao kupitia shindano la la "Jishindie Mamilioni" kwa wateja wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.


Akizungumza na na Vyombo vya Habari leo Meneja Mafunzo na Uwezeshaji wa SBC Rashid Chenja ni alisema kuwa ni vizuri kukumbuka kuwa Kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, michezo na afya, ambapo tangu mwaka 2013 kampuni hiyo imekuwa ikisaidia masgindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kama "Kombe la Meya" kwa Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.


"Mwaka huu tumeamua kuwaletea shindano kabambe lenye zawadi kemkem za fedha taslim, ambapo Shindano hili la "Jishindie Mamilioni" litaendeshwa kwa muda wa wiki sita kuanzia Aogosti 1, hadi Septemba 16 Mwaka huu katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Tabaora, Geita, Kigoma na Kagera," alisema.


Pia kwa upande wake Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa Hussein Mkwawa alisema kuwa shindano la "Jishindie Mamilioni" litakuwa na vizibo vya rangi ya silva, katika shindano hilo kutakuepo zawadi za pesa taslim kuanzia shilingi 1,000,000/-, 500,000/-, 10,000/-, 5,000/-, 1,000/- na Soda ya bure, ambapo ili mteja ajishidie zawadi ni lazima anunue soda za Pepsi, Mirinda, 7 Up zenye ujazo wa milimita 350 na milimita 300 kwa Mountain Dew.


Mkwawa alibainisha kuwa zawadi hizo mteja anaweza kuzipata ni shilingi milioni moja mpaka laki tano ambapo zitatolewa Kiwandani huku nyingine kati ya hizo zitatolewa hapo hapo uliponunulia kinywaji na katika gari ya mauzo.


Aidha Balozi wa Kinywaji cha Pepsi jijini hapa Albert G Sengo alisema mbali na hapo kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na Manispaa ya Ilemela katika kuhamasisha uchangiaji damu salama, ambapo amewaomba wateja kununua vinywaji hivyo kwa bei ya shilingi mia tano tu.

Post a Comment

0 Comments