Kocha wa England akaribia kutua Cameroon

Kocha wa England akaribia kutua Cameroon



Shirikisho la soka la nchini Cameroon (FECA FOOT) limethibitisha kufanya mazungumzo marefu na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven-Goran Eriksson kwaajili ya mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

Mazungumzo hayo yaliyodumu kwa takribani saa 72 yalifanyika wiki iliyopita kocha huyo alipotembelea makao makuu ya shirikisho hilo mjini Yoaunde.

“Tulimualika kocha huyo raia wa Sweden katika mazungumzo juu ya kazi ya kuifundisha timu yetu ya taifa ‘Indomitable Lions’ ambapo baada ya mazungumzo hayo na kuzingatia maombi ya makocha wengine tutatangaza kocha tuliyemchagua katika siku chache zijazo “. Imesema taarifa ya shirikisho hilo kupitia mtandao wa Twitter.

Nafasi hiyo ya kocha mkuu wa timu ya taifa, iliachwa wazi tangu mwezi Februari mwaka huu baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hugo Broos kumaliza mkataba wake.

Ukiachana na Eriksso, katika siku za karibuni pia kumekuwa na tetesi za baadhi ya makocha kadhaa wakubwa barani Ulaya kutajwa kuirithi mikoba hiyo ya Hugo Broos, makocha hao ni pamoja na mchezaji wa zamani wa AC Milan, Clarence Seedorf na Patrick Kluivert.

Sven-Goran Eriksson (70) sio mgeni katika soka la Afrika kwani alishawahi kuiongoza Ivory Coast katika michuano ya kombe la dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini na mafanikio yake makubwa katika timu za taifa ni pale alipoiongoza timu ya taifa ya Uingereza tangu mwaka 2001 hadi 2006.

Mara ya mwisho kocha huyo aliifundisha klabu ya Guangzhou Evergrande ya nchini China mwaka 2013 kabla ya kluhamia katika klabu ya Shanghai SIPG, amekaa nje ya kazi hiyo tangu Juni 2017.

Post a Comment

0 Comments