Mafanikio ni kitu cha lazima sana katika safari ya mjasiriamali. Uwe mjasiriamali mdogo, wa kati au mkubwa kwa vyovyote vile unahitaji mafanikio. Lakini ili kufanikiwa na kufikia mafanikio hayo, yapo mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyazingatia. Mambo hayo ni kama haya yafuatayo:-
1. Kujiwekea malengo.
Ukiwa kama mjasiriamali unayetakiwa kufikia mafanikio makubwa, suala la kujiwekea malengo ni lazima kwako. Unapokuwa na malengo yanakuwa yanakupa mwelekeo sahihi wa kupata kile unachokitaka.
Hiki ni kitu ambacho unahitaji kukizingatia sana kwani ni nguzo kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.
2. Kujitoa Mhanga(Take Risks)
Hakuna mafanikio makubwa utakayoyapata bila kujitoa mhanga. Wajasirimali wote wakubwa ni watu wa kujitoa mhanga sana. Wanakuwa wako tayari kutoa kitu chochote ilimradi wafikie malengo yao. Kitu cha kuzingatia hata kwako wewe unalazimika kujitoa mhanga na kulipia gharama ili kufikia mafanikio makubwa.
3. Kutokuogopa Kushindwa.
Wengi wetu tumefundiswa sana kuwa kushindwa ni vibaya. Hali ambayo hupelekea tunakuwa tunaogopa kujaribu karibu kila kitu kwa sababu ya hofu ya kushindwa.
Ikiwa wewe ni mjariamali unatakiwa kuwa jasiri na kujua kwamba mafanikio yanataka roho ya ujasiri na kutokuogopa kushindwa. Hiyo ndiyo siri itakayokifikisha kwenye kilele cha mafanikio na sio uoga unaouendekeza.
4. Acha kuridhika mapema.
Ni kosa kubwa sana kujikuta unaridhika mapema eti tu kwa sababu ya faida unayoitengeneza sasa. Ni vizri kujua, safari ya mafanikio bado ni ndefu kwako, hivyo hutakiwi kuridhika kwa namna yoyote ile. Kama kuna jambo umelifanikisha, endelea kwenye jambo lingine hadi kujenga mafanikio makubwa kabisa.
5. Tafuta ‘Mentor’
Acha kujidanganyai kuingia kwenye safari ya mafanikio huku ukiwa peke yako. Ikitokea umekwama kwa sababu huna mtu wa kukuelekeza au kukushauri, huo ndiyo unakuwa mwisho wako. Hivyo ni muhimu kuwa na kiongozi wako ‘mentor’ ambaye atakuongoza kwenye kufikia mafanikio yako.
0 Comments