Rais Magufuli awataka Viongozi kusimamia vema utekelezaji wa Ilani

Rais Magufuli awataka Viongozi kusimamia vema utekelezaji wa Ilani



RAIS Dk.John Magufuli amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kusimamia vema utekelezaji wa Ilani.

Amesema kuna watendaji wa Serikali ambao wamekuwa wakidai hawawezi kufuata Ilani kwa madai ya kuwa wapo Neutral na kwamba katika hilo hakuna Neutral kwani lazina Ilani itekelezwe.Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa tukio la kuwaapisha wakuu wa mikoa, Makatibu wakuu,manaibu makatibu wakuu pamoja na makatibu tawala ambao aliwateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hivyo baada ya kuwaapisha viongozi hao Rais Magufuli amehimiza utendaji kazi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuwatumikia vema Watanzania.
Amesema kuwa nchi yetu idadi ya watu ni milioni 55 hivyo waliopata nafasi imetokana na mipango ya Mungu na si kwa matakwa yao.Ameongeza kila aliyekuwa kwenye nafasi atambue yupo hapo kwasababu Mungu ameeamua na hata yeye kuwa Rais ni mpango wa Mungu.

Hivyo amewataka viongozi wote kwa ngazi mbalimbali kuanzia juu mpaka chini kila mmoja kwa nafasi yake afahamu yupo hapo kwasababu Mungu ametaka iwe hivyo na lazima wafanye kazi.Wakati anahimiza utendaji kazi na ushirikiano ameeleza umuhimu wa watendaji wa Serikali kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu.

Post a Comment

0 Comments