Kocha wa Manchester United Jose Mourinho usiku wa kuamkia leo alifanya Press baada ya mchezo wao dhidi ya klabu yake ya zamani Real Madrid huko Miami nchini Marekani katika mfululizo wa michezo ya kirafiki inayoendelea kwa vilabu mbali mbali.
Manchester United imecheza tayari michezo mitano ya kirafiki, huku baadhi ya michezo hiyo ikicheza na klabu mbili za kimarekani ambazo ni Club America Phenex ambapo matokeo yalikuwa sare ya 1-1,mchezo mwingine ni baina ya San Jose matokeo yalikuwa suluhu ya bila kufungana na mchezo mwingine ulikuwa baina ya AC Milan ambapo matokeo yake yalikuwa sare ya 1-1 lakini baada ya kuingia kwenye penati manchester walishinda kwa penati 9-8.
Mchezo mwingine ulikuwa dhidi ya wapinzani wao wakubwa Liverpool na katika mchezo huo United alipoteza kwa kipigo cha goli 4-1,lakini mchezo wa jana usiku United walileta matumaini kwa mashabiki wao kwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Real Madrid.
Baada ya mchezo huo Mourinho aliongea mengi sana akianza kwa kuwasifia vijana wake kwani wamepata ushindi dhidi ya timu kubwa na Mourinho kudai kwamba bado kikosi chake hakijakamilika hivyo wachezaji wote wakijumuika na wenzao atakuwa na matumaini zaidi.
lakini alipoulizwa swali kuhusiana na mchezaji wake ambaye majuzi aliondoka kwenye kambi ya timu kwenda kwao Ufaransa kwa ajili ya kuungana na mke wake wakati anajifungua mtoto wao wapili Anthon Martial.
Mourinho alisema “Anthony Martial? Ni bora kwa [afisa wa vyombo vya habari] Karen Shotbolt kujibu kama anataka kujibu, “Mourinho alisema. Shotbolt kisha akajibu:” Tuko hapa kuzungumza kuhusu mchezo na sio kuhusu Martial”
Alipoulizwa na mwandishi mwingine endapo kama Martial ataungana na wenzake kwa maana ya kurudi katika mazoezi Manchester, Mourinho alisema: “Sijui.”
Wakati huo huo, Phil Jones, Marcus Rashford na Romelu Lukaku wameamua kusitisha likizo zao ili kuja kuungana nasi katika mafunzo kabla ya msimu kuanza, Mourinho alisema.
Wachezaji hao watatu, ambao wote waliotajwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia, watarudi siku tatu zijazo mapema tofauti na ilivyopangwa ili kujiweka tayari kwa mchezo wa kwanza wa United dhidi ya Leicester City, Agosti 10.
0 Comments