Sababu ya Wanariadha kutoka Tanzania kulala Uwanja wa Ndege Nigeria hizi

Sababu ya Wanariadha kutoka Tanzania kulala Uwanja wa Ndege Nigeria hizi



Zaidi ya wanariadha 300 wakiwemo wa Tanzania na Kenya na kutoka mataifa mengine ya Afrika wamekwama katika uwanja wa ndege wa Murtala Muhammad 2 mjini Lagos Nigeria.

Kwa mujibu wa BBC, Wanariadha hao walitarajiwa kushiriki kwenye mbio za riadha za Afrika zitakazoanza leo.

Jumatano, mjini Asaba, jimbo la Delta, Nigeria. Ingawa mbio hizo zitang'oa nanga leo, matayarisho yalianza mwezi Novemba mwaka wa 2017.

Kikosi cha Zambia kilichowasili Nigeria siku ya Jumamosi, kimlifika uwanja wa mashindano siku ya Jumanne.

Mji huu wa Asaba ulitarajiwa kujizolea sifa kwa kuandaa Makala ya 21 ya riadha barani, lakini kuanzia siku ya jumamosi wiki hii, wanariadha kutoka matafa 52 wamekabiliwa na changamoto za uchukuzi na za usimamizi.

Wanariadha wa Kenya ndio walioathirika Zaidi huku Zaidi ya wanariadha 40 wakisalia uwanja wa ndege wenzao wakifanya mazoezi uwanjani wa Lagos.

Wengine wamegeuza uwanja wa ndege kuwa chumba cha malazi na uwanja wa kupiga jaramba. Wameonekana wakijinyoosha kwenye maeneo ya kuabiri ndege.

Tatizo hili limezidi mpaka baadhi ya wanariadha wamelazimika kutumia njia mbadala kama usafiri kwa gari na kuhatarisha usalama wao.

Post a Comment

0 Comments