Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa, amewajibu baadhi ya wanachama Simba wanaopingana na katiba ya mwaka 2018 baada ya kufanyiwa usajili siku kadhaa, na kudai kuwa kama wana malalamiko ,wanapaswa kufuata taratibu rasmi za kupinga na si kuzungumza kwenye vyombo vya habari.
Akizungumza na www.eatv.tv Msajili amesema katiba ya Simba ilijadiliwa katika mkutano mkuu wa klabu na kufuata taratibu ambapo pia ilipitia kunako makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na baadaye kuwalisishwa serikalini.
“Kutokana na kufuata kila taratibu juu ya usajili wa katiba hiyo, ni rasmi sasa itatumika katika uchaguzi mkuu ujao Simba bila mapingamizi yoyote yale kutokana na kujikamilisha kwake”, amesema Mkwawa.
Licha ya kuipokea katiba hiyo, wanachama hao wamepingana na baadhi ya vipengele ambavyo wameeleza kuwa havikuwa katika makubalino ya pande mbili baina ya viongozi na upande wao.
Wanachama hao baadhi wamekuwa wakipingana na katiba hiyo kutokana na baadhi ya vipengele ikiwemo mgombea Urais kutakiwa kuwa na kiwango cha elimu ya shahada badala ya kuishia kidato cha nne kama ilivyokuwa inayesma ya mwaka 2014.
0 Comments